HAKIKA RIADHA IMESAHAULIKA

Na Peter Akaro

Malcolm Forbes  aliwahi kusema kushindwa ni mafanikio kama tutajifunza kwenye hilo,ni wazi Tanzania kwenye mchezo wa riadha tumeshindwa tena kwa kiasi kikubwa,je tunatambua hilo na kutaka kujirekebisha?,jibu rahisi ni hapana.

Wiki iliyopita mashindano ya riadha ya Kili Marathon yalifanyika mjini Moshi,yalikuwa ni mashindano ya 14 kufanyika,huku tukishudia Wakenya waking’ara katika mashindano hayo kama ilivyo desturi yao.

Ninaposema riadha imesahaulika,nimetumia kigezo cha kawaida tu,kwa kutazama namna mashindano ya Kili Marathon yalivyofanyika.Licha ya kuwa mashindano makubwa yaliyojumusha wanaridha kutoka zaidi ya nchi 45 dunia,bado najiuliza thamani ya mashindano haya kwetu ipo wapi.

Mpaka mashindano haya yanafanyika sikuona wala kusikia yakizungumziwa au kupewa nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari hapa nchini,kama kuna mchezo kati ya Simba na Yanga,basi wiki ya tukio utasikia mashabiki wa timu hizi na viongozi wao wakitambiana kwenye vyombo habari,ilimradi kutengeneza hali ya upekee katika mchezo.

Mbona hili  halikufanyika Kili Marathon?,kuanzia kwa viongozi wa riadha,serikali,wadau wa michezo na vyombo vya habari ulikuwa wajibu wao kufanikisha hilo,sikitiko langu ni kwamba Kili Marathon imekuja kimya kimya na kuondoka kimya kimya,lakini ni kweli watanzania hatujui thamani ya mashindano haya?.

Kuna akili ya kitoto inaniambia huenda mzamini na yeye ameshakaitshwa tamaa na mwenendo wa riadha hapa nchini,mzamaini huyu ndo Yule anayedhimini pambano la Simba na Yanga maarufu kama mtani jembe,na utuaji wa tuzo za muziki maarufu kama KTMA,ukiangalia hivi vitu viwili mzamini huvitangaza sana kwenye vyombo vya habari na kwingineko,lakini mbona hafanyi hivyo kwa Kili Marathon?,hilo ni swali la kitoto lililoletwa na akili ya kitoto.

Wakenya ndo wanajua thamani na utamu wa mashindano haya,ndio wanajua,kama mbio za KM 45 kwa wanaume na wanawake medali zote wamechukua wao,na mbio za KM 21 katika zile nafasi 6 za zawadi(kwa wanaume na wanawake)  watanzania wawili tu ndo walioambulia,nafasi zote 4 wakachua wao,kwa nini wasijue utamu wa mashindano haya,kama wanaridha zaidi ya 250 wametoka Kenya wakaja  kushiriki ni wazi wanajua thamani ya mashindano haya.

Wakati anafunga mashindano hayo waziri mwenye dhamana ya michezo Nape Nnauye aliwashukuru sana waandaji wa mashindano hayo kwani wamesaidia kutangaza utalii wa mlima Kilimanjaro,kwa upande wake alikuwa sahihi akiwa kama kiongozi wa serikali,huenda ndo kitu  pekee cha kujivunia kutoka kwenye mashindano hayo kwa wakati huu ni utali,kama kutakuwa na lingine usisite kuniambia.

Lengo kuu la mashindano haya ni kuinua mchezo wa riadha na kuwaleta watu pamoja,ndo maana kuna mbio za kujifurahisha,swala la utali nafikiri linachukua nafasi ya pili,je lengo kuu limefikiwa?,na kama limefikiwa ni kwa asilimia ngapi?,maswali haya yananiacha njia panda.

Baada ya mashindano haya kumalizika viongozi wa riadha nchini wana nini cha kujivunia kwa sasa?,zaidi ya kuandaa,wakati wa kufunga mashindano hayo rais wa shirikisho la riadha Tanzania RT,Anthony Mtaka alimwambia waziri mwenye dhamana ya michezo Nape Nnauye,changamoto kubwa inayowakabili ni matokeo katika mashindano hayo,yaani wanariadha wa Tanzania kutofanya vizuri,huku (akijitetea) wanzentu wanajiandaa sana.

Kwa maana hiyo tunatka kujitete sisi hatukujindaa ndo sababu ya kushindwa,swala maandalizi nani anapaswa kulifanya?,zaidi ya shirikisho na wanaridha wenyewe,kama hiyo haitoshi,hatukufahamu mashindano yako mbioni kufanyika.

Mmoja kati ya washindi kutoka Kenya,alisema Tanzania kuna sehemu nzuri sana kujifunzia(mazoezi) kama mlima Kilimanjaro na sehemu nyingine zenye milima.

“Na kama imekua ngumu tunaomba mamlaka ya uamiaji Tanzania kwa sababu ni ndugu zetu,watume wanariadha waje kujifunza Kenya kwenye maeneo tofauti,wengine wajifunze Meru,wengine Kenya Uguru,na wakienda ng`ambo watakuwa wakimbiaji wazuri” alisema mshindi huyo.

Huenda hawa mwenzetu wanatushangaa kwa nini hatufanyi vizuri wakati tuna kila kitu!!!!.Na mashindano yakawa yameishia hapo,Wakenya wakapanda ndege kurejea kwao na medali kibao

SUDANI KUSINI MWANACHAMA MPYA WA EAC

Wakuu wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameikubalia Sudan Kusini kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ya kikanda.
Mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo jijini Arusha jana Jumatano (Machi 2) umepitisha pendekezo la baraza la mawaziri juu ya uwanachama wa Sudan Kusini na pia hali ya usalama nchini Burundi.

Kikao hicho kilichodumu kwa muda wa takribani masaa matano kimelikubalia taifa hilo changa kabisa barani Afrika kuwa mwanachama wake wa sita, kuungana na Tanzania, Rwanda, Burundi , Uganda
na Kenya.

Rais Magufuli ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho, amewaambia wajumbe wa mkutano huo wa kilele kwamba sasa "Sudan ya Kusini ni mwanachama halali wa jumuiya" hiyo.

Mkutano huo pia umezungumzia kwa kina masuala ya maendeleo ndani ya jumuiya ikiwemo mipango ya kujengwa kwa viwanda vya nguo na bidhaa za ngozi ili kuondoa kabisa biashara ya uagizaji wa nguo kuukuu, maarufu kama mitumba, katika nchi hizo katika miaka michachache ijayo

Mkutano huo pia umeshuhudia uzinduzi wa pasi ya kusafiria ya kielektroniki itakayotumiwa katika eneo la Afrika Mashariki pamoja na mwongozo maalum wa kimaaadili katika biashara kwenye nchi wanachama wa jumiya hiyo.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya jumuiya hiyo, Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Dk. Richard Sezibera, amesema kuwa jumiya hiyo inasonga mbele kwani itifaki mbalimbali zimepitishwa kuanzia ushirikiano katika soko la pamoja, ushuru wa forodha na sasa wanaelekea kufikia hatua ya Afrika Mashariki kuwa na sarafu moja itakayotumika katika nchi zote wanachama.

Amesema kuwa tayari jitihada zinaendelea katika kuondoa vikwazo mbalimbali katika sekta za mawasiliano, biashara na usafiri "ili kuwapa wananchi wa Afrika Mashariki fursa ya kuufurahia na kufaidi muungano" huo.

Katika mkutano huo, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi hakuhudhuria na badala yake alimtuma makamu wake wa pili, Joseph Butore, huku serikali ya Sudan Kusini ikiwakilishwa pia na makamu wa pili wa rais, James Waniiga.

Na katika hatua nyingine kikao hicho kimepitisha jina la Liberate Mfumukeko kutoka Burundi kuwa katibu mkuu mpya wa jumuiya hiyo kuanzia Aprili 1 mwaka huu.

WASANII KIBAO KUKINUKISHA KWENYE 'AMSHA MAMA FESTIVAL' JMOSI HII

Wasanii   mbalimbali wa muziki hapa nchini, Jumamosi hii wanatarajiwa kukinukisha vilivyo katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, katika tamasha la Amsha Mama Festival.

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake, Balozi wa tamasha hilo Khalid Ramadhani ‘Tundaman’, ambaye amepewa Ubalozi huo kupitia waandaaji wa tamasha la (AFWAB) AMSHA MAMA Festival 2016, lililo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya Candy na Candy Records Joe Kariuki, alisema tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Machi 5 mwaka huu katika uwanja wa Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

Tundaman na Muandaaji wa tamasha hilo Kariuki, wamesema kwamba maandalizi ya shoo hiyo tayari yameshakamilika kwa kiasi kikubwa hivyo angependa kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa jiji la Dar, kujumuika siku hiyo kushuhudia burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii kibao ambao tayari wemedhibitisha kufanya makamuzi siku hiyo.

“Tunapenda kuwaalika Watanzania wote kwa ujumla siku ya jumamosi hii ya Machi 5, mwaka huu waje kwa wingi katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar Salaam, ili tujumuike kwa pamoja katika tamasha la kuhamasisha wanawake kujikwamua katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.

Tamasha hili litakuwa ni la wazi kwa maana kwamba watu wote watapata burudani kibao bila malipo yaani bure kabisa hivyo waje kuwashuhudia wasanii kama, Khadija Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky na Tunda Man wakitoa burudani ya hali ya juu kwani ulinzi na usalama siku hiyo ni wa uhakika,” alisema Tunda Man.
Kwa upande wake, Joe

Kariuki ambaye ni mratibu mkuu wa tamasha hilo ametumia muda huu kuongea na baadhi ya akinamama wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali hususani mama ntilie, wauza matunda na wauzaji wa mitumba ili nao wajitokeze kwa wingi kuja kunadi bidhaa zao siku hiyo kwani hiyo ndiyo fursa yao ya kipekee ya kkujitangaza bure.

MTULIA AMPINGA MAKONDA

Mbunge wa Kinondoni, (CUF), Maulid Mtulia amepinga mpango wa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusafiri bure kwenye daladala akisema utawashushia heshima.

Badala yake, alitaka Manispaa ya Kinondoni iweke utaratibu wa kuwaongezea walimu fedha za usafiri kwenye mishahara yao ili wajilipie wenyewe.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Paul Makonda kutangaza kuwa walimu wa shule za Serikali za Dar es Salaam watasafiri bila kulipa nauli kwenye daladala.

Katika mpango huo ambao umepangwa kuanza Jumatatu ijayo unaozigusa pia manispaa za Temeke na Ilala, walimu watapatiwa vitambulisho maalumu vyenye saini ya Makonda.

Akizungumza katika mahojiano maalumu juzi, Mtulia alisema licha ya kuwa wazo lililenga kuwasaidia walimu, lakini litawasababishia dhihaka.

Alisema kinachopaswa kufanyika ni kutafuta suluhisho la kudumu la kero zinazowakabili walimu ambazo zinachangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.
“Itafika hatua kondakta atamsimamisha mwalimu kwenye kiti kama ilivyo kwa wanafunzi kwa sababu tu halipi nauli… Wazo hili ni zuri lakini lilipaswa kuboreshwa kama kweli nia ni kumsaidia mwalimu,” alisema.

Alisema ikiwa kweli nia ni kuwasaidia walimu, basi halmashauri zina wajibu wa kuhesabu siku za kazi na kiasi ambacho mwalimu atalipia nauli ili fedha hizo ziongezwe kwenye mshahara wake.

Alisema njia hiyo itakuwa ya heshima zaidi kuliko walimu kusafiri bure kwa kutumia vitambulisho kama walivyo wanafunzi wao.
Hata hivyo, alisema ipo haja kwa viongozi wa manispaa hiyo kukaa meza moja na walimu ili kujua changamoto zinazohitaji suluhu ya haraka, akisema huenda nauli ikawa si ya msingi kwao.

SLAA AFUNGA NDOA CANADA

Aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.

Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka
20 iliyopita.

Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani akidai bado anamtambua Josephine kuwa ni mke wake wake halali.

Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.

Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.
Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi 
hayo.