Askofu wa
kanisa la ufufuo na uzima Joseph Gwajima aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya
TMJ ya jijini Dar es saalam baada ya kuugua ghafla wakati akifanyiwa mahojiano
na jeshi la polisi,ameachiwa kwa dhamana na jeshi hilo huku akitakiwa kufika katika
kituo kikuu cha polisi april 02,2015 kwa ajili ya kuendelea na mahojiano na
jeshi la polisi.
Taarifa
za awali zilikuwa zinasema kwamba askofu Gwajima angefikishwa kituo kikuu cha
polisi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuendelea kuhojiwa na jeshi la polisi
kutokana na kusitishwa kwa mahojiano hayo baada ya kuugua ghafla na kulazwa
katika hospitali ya TMJ jambo ambalo lilisababisha wafuasi wake kuanza
kukusanyika kituoni hapo huku askari polisi wakitumia nguvu ya ziada ya
kidiplomasia kuwatawanya.
Hata
hivyo majira ya saa saba za mchana kukawepo na taarifa mpya za askofu Gwajima
kufikishwa katika kituo cha polisi cha Osterbey kilichopo katika mkoa wa
kipolisi wa kinondoni na kushuhudia umati mkubwa wa askofu huyo ukiwa nje ya
kituo hicho huku baadhi ya askari wa kituo hicho wakiwa na silaha wakiranda
randa katika eneo zima la kituo hicho wakati askofu huyo akiwa ndani ya kituo
hicho cha polisi.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment