Mwandishi Eva Mbesele (TSJ).
Waandishi wa habari hususani ambao
bado wapo vyuoni wametakiwa kuwa wabunifu pamoja na kuiheshimu taaluma yao ili
waweze kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye soko la ajira katika sekta ya habari ambayo inakua kwa kasi hapa
nchini.
Geti kubwa la kuingia kwenye ofisi za shirika la utangazaji Tanzania TBC zilizopo Bamaga jijini Dar es salaam
Wito huo umetolewa leo na Angela
Man’genya ambae ni mhariri
wa habari za Redio katika shirika la utangazaji
Tanzania TBC wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari
Time School of Journalism (TSJ) walipotembelea
ofisi za shirika hilo zilizopo Bamaga
jijini Dar es salaam kwa ziara ya
kimasomo
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha uandishi wa habari (TSJ) wakiwa mapokezi wakisubiri utaratibu wa kuingia kwenye ofisi za TBC kwaaji ya ziara ya kimasomo
Aidha Man’genya aliongeza kuwa wanahabari ambao bado
wapo vyuoni wanatakiwa kusoma kwa bidii na sio kwenda chuo kuonyeshana ufahari
wa mavazi kwani tasnia ya habari inakua kwa kasi sana na inahitaji watu ambao
wamesonma.
“Waandishi wa habari mnatakiwa kuwa wabunifu na kujituma sio kusubiri mpaka upanangiwe kazi” Alisema
Man’genya.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari (TSJ) wakiingia kwenye ofisi za shirika la utangazaji Tanzania TBC
Katika ziara hiyo wanafunzi hao
walijifunza vitu vingi ikiwemo jinsi ya kuandaa habari, kusoma habari, kuhariri
vipindi vya Radio pamoja na Luninga napia walitembelea sehemu mbalimbali ndani
ya ofisi za shirika hilo zikiwemo chumba cha kufanyia vipindi mbalimbali,
chumba cha kupokelea matangazo ya nje, chumba cha kuhariri habari na chumba cha
kusomea taarifa za habari.
Baadhi ya wanafunzi wa (TSJ) wakiwa kwenye studio ya kufanyia vipindi kwenye ofisi zashirika la utangazaji Tanzania TBC
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari (TSJ) wakipata maelekezo kwenye chumba cha habari cha TBC
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari (TSJ) wakiwa kwnye chumba cha kurushia matangazo ya television kwenye ofisi za shirika la utangazaji (TBC)
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari (TSJ) wakiwa kwenye chumba maalumu cha kusomea taarifa za habari katika ofisi za shirika la utangazaji Tanzania TBC







No comments:
Post a Comment