BARCA WAINGIA PABAYA

Siku chache baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup, Barcelona wamekiona cha moto baada ya kukutana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Athletic club Bilbao.

Licha ya kuwemo kwa nyota Leonel Messi, Bilbao walitoa  adhabu hiyo kwa Barcelona katika mechi ya Super Cup ya Hispania iliyopigwa jana usiku
Hadi mapumziko, Bilbao walikua wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mikel San Jose  katika dakika ya 13,
Huku ikionekana Barcelona ingerejea na kujirekebisha katika kipindi cha pili kama ilivyofanya kwenye mechi ya Super Cup dhidi ya Sevilla baada  ya kutangulia kufungwa na kusawazisha, haikuwa hivyo.

Kwani Bilbao ndiyo walizidi kupaa na kufunga mabao ya harakaharaka baada ya Artiz Aduriz kufunga mabao mawili ya haraka katika dakika ya 53 na baadaye 63.
Kitendo cha Bilbao kufikisha mabao matatu kilionekana kuwachanganya Barca, wakaendelea kushambulia mfululizo na kujisahau kufanya ulinzi mzuri.

Hali hiyo ilisababisha Bilbao kupata bao la nne kupitia Aduriz aliyekuwa anafunga bao  lake la tatu katika mchezo huo (hat trick.)
Barcelona walijariba kuingiza nyota wake kama Iniesta, Mascherano na Raktic walionzia benchi lakini hawakuweza kuisadia timua yao kubadilisha matokeo.

No comments: