RAIS KIKWETE AAHIDI KUENDELEA KUWALEA NA KUWAPIGANIA WASANII NCHINI

Rais Jakaya Kikwete amesema ataendelea kuwa mlezi wa wasanii hata baada ya kumaliza muda wake wa uongozi.

Rais Kikwete ameyasema hayo katika hafla maalum ya kumuaga  na Muungano wa Wasanii wa Tanzania waliokuwa wakimuaga na kumshukuru kwa ushirikiano mkubwa wakati wa uongozi wake.

Katika hafla hiyo iliyofana kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Kikwete aliwaambia wasanii yuko tayari kuendelea kuwa mlezi wao.
“Nitaendelea kuwa mlezi, ningependa kuifanya kazi hii baada ya kustaafu. Ninaamini nitakuwa bado ni mwananchi mwenye jina.
“Kama nitaingia sehemu na kupiga hodi, nikazungumzia jambo fulani kuhusiana na wasanii, ninaamini nitasikilizwa.

“Hivyo nitaendelea kuwapigania kadiri ya uwezo wangu. Lakini kabla ya Oktoba, nitajitahidi mambo kadhaa niyatimize kwa kuwa hadi sasa kuna baadhi ambayo  kwa kushirikiana nanyi,” alisema Kikwete.
Wasanii mbalimbali walizungumza pamoja na  kutumbuiza katika hafla hiyo na Kikwete alikabidhiwa picha yenye sura yake ambayo ina majina ya wasanii mbalimbali.

No comments: