Na Peter Akaro
Wakali wa R&B kutoka kwenye Bongo
flava,Jux na Ben Paul
wameuzungumzia wimbo wao mpya
unaokwenda kwa jina la 'Nakuchana'
waliouachia hivi karibuni.
Wimbo huo uliofanyika katika studio
za AM Record na producer Maneke,ni
wa mahadhi ya kujibizana kati ya wawili
hao,huku kila mmoja akimchana
mwenzake kuhusu mambo flani.
Akizungumzia kolabo hiyo Ben Paul
alisema kila mstari katika wimbo huo
waliandika pamoja na walitaka
kufanya kitu cha kipekee sana ila
wakaona ngoja wacheze na studio
waonyeshe uwezo wao wa sauti.
"Hata wimbo ulivyotoka na jinsi
tunavyopata mrejesho kutoka mtaani
tunashangaa huu wimbo umebamba
kiasi hiki,juzi nilikuwa na 'show'
Arusha namaliza kuimba watu
wanataka (nakuchana)" alisema Ben Paul.
wimbo huo ambao umekuwa kivutio
kwa mashabiki hasa Jux
anapomchana Ben Paul hajui kuvaa
na huku Ben Pau akimchana Jux kuwa
anatumia pesa alizoachiwa na
aliyekuwa mpenzi Jack ambaye kwa
sasa anatumikia kifungo jela nchini China.
Kwa upande wake Jux alisema wao
wanacheza na maneno na namna
watu wanavyokuwa wanaandika
ndivyo sivyo katika mitandao na si
vinginevyo.
Jux anaongeza kwa kusema
mashabiki walikuwa wanaongea vitu
vingi sana,tukaona vitu vingine
tukiviweka katika wimbo vitawapa
mashabiki utayari na kuchukulia kwa
umakini.
"Lilipotokea swala la Jack kuna mambo
mengi yaliongelewa nyuma,mashabiki
walingea vitu vingi sana,kwa hiyo
alichomaanisha Ben Paul sio pesa na
mavazi alikuwa ananipa(jack) bali zile
kiki ndo zilifanya mimi ning'ae"
alisema Jux.
Walipoulizwa mbona wimbo wao
umefanana na wa Bob Mapesa-
Utamu kutoka kenya,Ben Paul alisema
hawajaiga wimbo ila kwenye mziki
kuna vitu huwa vinafanana.
No comments:
Post a Comment