Jamie Vardy aliwafungia Leicester mabao mawili na kuwawezesha kuilaza Liverpool na kuendelea kung'ang'ania kileleni mwa ligi kuu ya England kwa tofauti ya pointi na klabu ya Man city.
Mshambuliaji huyo Mwingereza alifunga bao la kwanza kwa shuti kali la mita 25 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Riyad Mahrez dakika ya 60.
Vady aliihakikishia ushindi timu yake baada ya kufunga bao la pili kwenye dakika ya 71 baada kuunganisha vema pasi ya wa Shinji Okazaki .
Kwingineko, Arsenal walilazimishwa sare tasa na Southampton nyumbani, jambo lililowafanya kupitwa na Tottenham katika msimamo wa ligi hiyo.
Manchester United hata hivyo walitamba kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Stoke City uwanjani Old Trafford, mabao yao yakifungwa na Jesse Lingard (14’), Antony Martial (23’) na Wayne Rooney (53’).
Ligi hiyo inaendelea tena usiku wa leo ambapo Chelsea watakuwa ugenini Watford, nao Everton watakuwa nyumbani Goodison Park kuikaribisha Newcastle.
Matokeo ya mechi za Jana.
Arsenal 0 -0 Southampton
Leicester 2-0 Liverpool
Norwich 0-3 Tottenham
Sunderland 0-1 Man City
West Ham 2-0 Aston Villa
Crystal Palace 1-2 Bournemouth
Man Utd 3-0 Stoke
West Brom 1-1 Swansea.
No comments:
Post a Comment