Floyd Money Mayweather amesema kuwa amepewa fedha chungu nzima ili kumshawishi arudi katika ulingo wa ndondi.
Lakini licha ya kupewa fedha hizo ,Mayweather ambaye alistaafu baada ya pigano lake la 49 mnamo mwezi Septemba hana mpango wa kurudi ulingoni.
”Kwa sasa hivi ,nimeamua kustaafu kabisa”,alisema bingwa huyo mwenye umri wa miaka 38.
”Iwapo nitahisi kurudi,haitakuwa sababu ya kutaka fedha”,lakini ni lazima nilipwe,hiyo ndio maana ya jina lango Money Mayweather”.
Mayweather ameshinda mataji ya dunia katika mizani mitano tofauti kabla ya kustaafu na rekodi nzuri.
No comments:
Post a Comment