WHO WATOA TAHADHARI JUU YA HOMA YA ZIKA

Kamati ya dharura ya miongozo ya kimataifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), iliyokutana Jana  mjini Geneva, Uswisi kufanya tathmini ya ugonjwa wa ZIKA imetoa taarifa kuwa ugonjwa huo unasambaa kwa kasi sana duniani.

Wataalam wa maswala ya afya wa shirika hilo wanahofu kuwa virusi vinasambaa mbali na kwa haraka,vikisababisha madhara makubwa,
maambukizi yamekuwa yakihusishwa na maelfu ya watoto wanaozaliwa wakiwa na vichwa vidogo .

Tahadhari ya WHO kuhusu Zika ni ya hali ya juu sawa na ya Ebola, hii inamaanisha kuwa utafiti na misaada itatolewa kwa haraka kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Mkurugenzi mkuu wa WHO, Margaret Chan amesema nguvu ya pamoja inahitajika kupambana na virusi hivyo
amesema masuala yanayopewa kipaumbele ni kuwalinda wanawake wajawazito  dhidi ya mbu wanaosambaza virusi vya Zika.

Tangu mwezi Oktoba kumekuwa na ripoti ya kesi 4,000 za watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo nchini Brazil pekee, tatizo hili linatajwa ni moja ya athari za virusi vya homa ya Zika.

No comments: