WAKAZI
10 wa jijini Tanga, akiwemo mwanafunzi wa sekondari wamefikishwa mbele
ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wakikabiliwa na makosa matano tofauti kuhusu
tukio la kuwanyang’anya polisi silaha pamoja na kumuua askari wa Jeshi
la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Sajenti Mohamed Rashid Kajembe.
Mwanafunzi aliyefikishwa mahakamani ni Rajab Bakari (19) wa shule ya sekondari na mkazi wa Makorora jijini hapa.
Watuhumiwa
tisa wameelezwa kuwa ni wafanyabiashara, nao ni Mbega Seif (25) maarufu
‘Abuu Rajab’ mkazi wa Kiomoni, Amboni, Ayubu Ramadhani (27) maarufu
‘Chiti’ ambaye ni fundi umeme na mkazi wa Kona Z Kiomoni, Hassani Mbogo
(20) maarufu ‘Mpalestina’ mkazi wa Makorora, Mohamed Ramadhani (19)
mfanyabiashara na mkazi wa Makorora, Sadiki Mdoe (25) maarufu ‘Kizota au
Kisaka’ mkazi Magaoni.
Washtakiwa
wengine ni Saidi Omari (26) mkazi wa Magaoni Tairi Tatu, Nurdin Mbogo
(27) Makorora, Ramadhan Mohamed (18) mkazi wa Donge pamoja na Omari
Harubu Abdala (55) maarufu ‘Ami’
Wakisomewa
mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Aziza Rutala, Wakili wa Serikali,
George Barasa akisaidiana na MariaClara Mtengule, walidai kuwa kosa la
kwanza hadi la tatu linawahusisha washitakiwa namba moja mpaka nane (1
-8) ambao wanatuhumiwa kushiriki kula njama ya kutenda kosa kinyume cha
sheria.
No comments:
Post a Comment