AL SHABAB WAUA 10 MOGADISHU

Watu 10 wameripotiwa kuuawa baada ya Kundi la wapiganaji linaloshukiwa kuwa sehemu ya wanamgambo wa Al Shaabab kuvamia hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.





















Kwa mujibu wa walioshuhudia wamesema kuwa 
 wapiganaji hao wa Al Shabaab walishambulia hoteli ya Maka al-Mukarama mjini Mogadishu moja katia ya hoteli maarufu mjini humo ambayo inapendwa na watu  wengi wakiwemo wafanyikazi wa kimataifa na mabalozi.


Kundi la Al Shaabab limekuwa likitekeleza mashambulizi ya aina hii katika hoteli zinazosifika kuwa mahala pa burudani kwa wageni na viongozi mashuhuri serikalini
Shambulizi hili la leo linafuatia lingine lililoanza kwa bomu yapata mwezi mmoja uliopita nje ya hoteli hiyo.















No comments: