MCHINA CHALI KWA MATUMLA

Bondia Mohamed Matumla Snake Jr wa Tanzania jana usiku alimchapa bondia Wang Xin Hua kutoka China kwa pointi katika pambano la raundi 10  la kuwania nafasi ya kucheza kwenye pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa masumbwi Duniani kati ya bondia Floyd  "Money"Maywether Jr wa Marekani na Manny Pacquiao wa Ufilipino litakalofanyika Mei Mwaka huu nchini Marekani.








































































Kwenye pambano hilo lililopigwa jana usiku kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee lilitanguliwa na mapambano mbalimbali likiwemo lile lililowakutanisha bondia Mada Maugo na Jaferty Kaseba wote wa Tanzania ambopo katika pambano hilo Maugo alishinda kwa Know Out ya raundi ya nane


Picha kwa hisani ya Michuzi Blog





No comments: