BREAKING NEEEEEEWZ!!! MTANDAO WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NIGERIA WAVAMIWA NA WAHALIFU

Huku mamilioni ya raia wa Nigeria wakipiga kura kumchagua rais mpya,tovuti ya tume ya uchaguzi nchini Nigeria imeingiliwa na wahalifu wa mtandaoni.



Kundi linalojiita Jeshi la mtandaoni la Nigeria limeweka ujumbe katika tovuti hiyo likiionya tume ya uchaguzi ya Nigeria dhidi ya kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo.
kufikia sasa haijulikani iwapo wahalifu hao wameingia zaidi ya mtandao huo japokuwa wamesema kuwa walikuwa wakithibiti data yote ya tume ya uchaguzi.
Tume hiyo imesema kuwa ina maelezo kuhusu shambulizi hilo la mtandaoni na sasa imeanza kufanya uchunguzi.
Ujumbe huo wa wahalifu hao wa mtandaoni pia unasema kuwa wameweza kuingilia data ya serikali.
Mitandao kadhaa maarufu ya serikali ya Nigeria imefungwa katika miaka ya hivi karibuni ukiwemo ule wa bunge.
Katika tukio jingine wananchi  wengi wa Nigeria wamechelewa kupiga kura ya kumchagua rais kutokana nakutokea matatizo ya kiufundi katika uchaguzi huo
Rais Goodlack Jonathan ni miongoni mwa watu walioathiriwa na tatizo hilo swala lililomfanya usubiri nje ya kituo cha kupigia kura kwa mda.
Raisi wa Nigeria Goodlack Jonathan akiongea na wanahabari mara baada ya kushindwa kupiga kura kutokana na matatozo ya kiufundi yaliyojitokeza




No comments: