Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo asubuhi imefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya taifa ya Malawi (The Flames) katika mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayochezwa kesho jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akiongea na waandishi wa habari leo kaika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri , na sasa kilichobakia ni mchezo wenyewe wa kesho.
Mayanga amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wachezaji wapo kwenye ari na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni kesho tu kushuka dimbani kusaka ushindi.
Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza, mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda), mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akiba Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka Mwanza.
Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika nafasi ya 91 kwenye vinago hivyo.
kocha msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga
No comments:
Post a Comment