Serikali wilayani IRINGA imeifunga shule ya Sekondari ya IDODI iliyopo
Tarafa ya Idodi kwa muda wa wiki mbili ili kutoa nafasi ya kufanyika
ukarabati na uchunguzi wa mfululizo wa matukio ya kuungua moto kwa
mabweni ya shule hiyo.
Tangazo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Angelina Mabula kufuatia tukio la kuungua moto kwa bweni jingine la wasichana la shule hiyo hapo jana ikiwa ni tukio la pili ndani ya mwezi mmoja.
Mkuu wa wilaya hiyo Angelina Mabula ametembelea shule hiyo kujionea hali
halisi huku akiwafariji wazazi na wanafunzi walioathirika na moto na
kutoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano.
Mkuu wa Shule ya Idodi, Mwalimu Christopher Mwasomola anasema agizo la
kufanya mabadiliko ya mfumo wa umeme yalifanyika lakini hayajazaa
matunda.
Moto huo umezua Taharuki kubwa kwa Wanafunzi na Wazazi na baadhi
wakihusisha na imani potofu na kutoa mapendekezo kwa serikali ikiwemo
kuangalia iwapo wananchi waliokuwa wanakaa eneo hilo kabla ya kuwa shule
wali ridhia kuondoka katika eneo hilo.
Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa mabweni ya Shule ya idodi kuungua baada
ya tukio la moto la mwaka 2009 lililogharimu maisha ya wanafunzi 12.




No comments:
Post a Comment