HUU NI MSIBA WA KITAIFA

Msetoblog inaungana na watanzania wote kutoa pole pamoja na salamu za rambirambi kwa ndugu zetu wote walioondokewa na wapendwa wao katika ajali mbaya ya basi la majinja express ambalo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam kufunikwa na kontena maeneo ya Changalawe, Mafinga mkoani Iringa. 

Ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi imesababisha vifo vya watu 42 na kujeruhi wengine 23





Mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na kuwapa uzima majeruhi wote waliopo hospitalini.





Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
Wote safari yetu ni moja cha msingi ni kuwaombea na kushikamana katika kipindi hiki kigumu







No comments: