China ni nchi yenye historia ndefu na utamaduni mkukbwa, na vivutio
vingi vya utalii. Kumbukumbu nyingi za mandhari ya kimaumbile na za
utamaduni zinadhihirisha akili nyingi na juhudi kubwa za watu wa China
ya kale. Mwaka 1985 serikali ya China ilijiunga na “Mkataba wa Urithi wa
Dunia”, na mwaka 1987, kumbukumbu 6 za urithi wa China ikiwa ni pamoja
na Ukuta Mkuu na Kasri ya Kifalme ya China viliwekwa kwenye orodha ya
urithi wa dunia.
Ukuta Mkuu unasifiwa kama ni “moja katika maajabu 7 ya dunia” ni jengo
kubwa ambalo lilitumia miaka mingi na kazi kubwa duniani, katika ngome zote za kuzuia maadui katika zama za kale. Ukuta huo una urefu wa zaidi
ya kilomita 7,000.
Historia ya ujenzi wa ukuta huo inaweza kufuatiliwa hadi karne ya 9
kabla ya Kristo. Katika kipindi cha “Madola Kivita” kilichokuwa kati ya
mwaka 770 K.K. na 476 K.K. madola yalikuwa yakipigana vita na kila moja
likitaka kuliangamiza lingine ili kupata utawala wa China nzima,
kutokana na sababu hiyo kila dola lilijenga ukuta milimani kwenye mipaka
ili kuzuia mashambulizi ya maadui. Mwaka 221 kabla ya Kristo, mfalme
Qin Shuhuang aliiunganisha China nzima, kisha akaziunganisha kuta zote
zilizojengwa na madola hapo awali na zikawa ukuta mkuu. Katika miaka
zaidi ya elfu mbili kila enzi ilizidi kuongeza urefu wa kuufanya ukuta
huo kuwa na kilomita elfu 50, urefu ambao unaweza kuizunguka dunia kwa
duara na zaidi kwa kufuata ikweta.


No comments:
Post a Comment