KAULI YA BAN KI-MOON KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Leo Ulimwengu unaadhimisha siku ya wanawake Duniani ambapo katibu mkuu wa umoja wa Mataifa bwana Ban Ki-Moon amesema madhila yanayowakumba wanawake, wasichana pamoja na watoto wa kike bado yanatikisa maeneo mbalimbali duniani


Ban Ki-Moon
Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa

Katika ujumbe wake wa siku hii ametolea mfano maeneo ambayo watoto wadogo wa kike wenye umri wa miaka saba wanatumiwa kama silaha ya vita na makundi yenye misimamo mikali ikiwa ni miongo miwili baada ya mkutano wa nne wa  kimataifa wa wanawake uliofanyika Beijing ukilenga pamoja na mambo mengine kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Kwa mantiki hiyo ameitaka Dunia kuungana dhidi ya makundi haya ambayo yapo Nigeria, Somalia,Syria na Iraq ambayo yamegeuza miili ya wanawake kuwa uwanja wa vita kwa lengo la kukidhi matakwa yao.
Boko Haram 
Moja kati ya makundi ya waasi  yenye msimamo mkali kutoka Nchini Nigeria







No comments: