KESHO NDIO KESHO HUKU EL CLASICO KULE MAN U NA LIVERPOOL

Kesho ligi kuu ya Hispania itaendelea huku mechi ambayo inatarajiwa kuteka hisia za mashabiki wengi wa soka duniani ni kati ya mahasimu wakubwa wa ligi hiyo Barcelona na Real Madrid ambazo zinatarajiwa kushuka dimbani kwenye dimba la Camp Nou .













Mechi hiyo maarufu kwa jina la El Clasico itaanza majira ya saa mbili za usiku kwa saa za Afrika mashariki. Katika mechi ya kwanza iliopigwa kwenye dimba la Santiago Benarbeu Real Madrid iliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja mabao yaliyofungwa na Ronaldo,Pepe pamoja na Karim Benzema huku lile la kufutia machozi la Barcelona likifungwa na Neymar
























Nchini England kwenye ligi kuu ya nchi hiyo kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Manchester United watako kuwa wageni wa Liverpool kwenye dimba la Anfield.


























Mechi hiyo itakayoanza majira ya saa kumi na nusu za jioni kwa saa za Afrika mashariki inatarajiwa kuwa kali na yakusisimua kutokana na upinzani pamoja na mafanikio ya timu hizo ndani na nje ya England.




























No comments: