Serikali ya Kenya imeutambua rasmi mwili wa mtu mmoja uliopatikana katika mbuga ya wanyama ya Tsavo, kuwa ni wa Meshack Yebei ambaye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili makamu wa rais wa Kenya William Ruto. kwenye Mahakama ya ICC.
Meshack Yebei
Mkemia wa serikali ya Kenya ametangaza kuwa mwili huo ambao ulikuwa
umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti tangu mwezi December mwaka 2014 ni
wa Meshack baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi wa chembechembe za DNA.
Meshack Yebei
Meshack Yebei alitekwa mwishoni mwa
mwezi December nyumbani kwake Eldoret alipokwenda kumwona mkewe
aliyekuwa anaumwa, familia yake ililalamika kuwa kutoweka kwa Yebei kunatokana na kuhusishwa na kesi hiyo.
William Ruto
Yebei alitarajiwa kuwa shahidi wa Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto kwenye kesi yake ya mauaji inayoendelea Mahakama ya ICC, The Hague.



No comments:
Post a Comment