KANDORO, MANYANYA WAMTEMBELEA MTOTO BARAKA HOSPITALINI

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro na mkuu wa mkoa wa Rukwa mhandisi Stella Manyanya wamemtembelea mtoto Baraka Cosmas ambae ni mlemavu wa ngozi aliekatwa kiganja cha mkono na watu wasiojulikana nyumbani kwao juzi


Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya, Dk. Mpoki Ulisubisya akiwaongozwa Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa kuelekea Wodini kumjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.

Mtoto huyo mkazi katika kijiji cha Ikonda kata ya Chitepa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa alihamishiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kukatwa kiganja chake akitokea kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani hapa.


Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa wakimjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo, Prisca Shaban(28) alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa saba usiku alipokuwa anarudi ndani akitokea nje kujisaidia alivamiwa na mtu ambaye hakumfahamu na kisha akamsukumia ndani kabla ya kumpiga kichwani kwa rungu na kisha kupoteza fahamu.


Mama mzazi wa mtoto Baraka,Prisca Shabani akiwa na jeraha kichwani baada ya kupigwa na watu waliomkata kiganja mtoto wake.


Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi akiwa amelala kitandani akiendelea kupatiwa matibabu.









No comments: