Mechi ya robo fainali ya kombe la FA kati Manchester united dhidi ya Arsenal imemalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja mabao ya Arsenal yamefungwa na Nacho Monreal pamoja na Danny Welbeck huku lile la kufutia machozi la Man utd likiwekwa kimiani na Wayne Rooney
Hata hivyo Man utd wamemaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao Angel Di Maria kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumsukuma mwamuzi
Mchezaji wa Arsenal Nacho Monreal( alieruka juu) akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza
Wayne Rooney wa Manchester Utd akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kusawazisha
Danny Welbeck akishangilia mara baada ya kuifungia Arsenal goli la pili na laushindi katika mchezo huo
Mwamuzi Michael Oliver akimuonyesha kadi nyekundu Angel Di Maria (mwenye bukta namba 7) baada ya Di Maria kumsukuma mwamuzi huyo

No comments:
Post a Comment