MKE WA ZAMANI WA RAISI WA IVORY COAST AENDA JELA MIAKA 20

Mke wa aliekua Raisi wa Ivory coast Laurent Gbagbo, Bi Simone Gbagbo amehukumiwa kifungo cha maika 20 jela na mahakama  kuu ya nchi hiyo kufuatia kesi iliokua inamkabili ya kuhusika katika vurugu zilizotokea kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wa mwaka 2010

Simone Gbagbo

Vurugu hizo zilizosababisha vifo vya watu zaida ya 300 zilitokea baada ya Bi Simone na mume wake ambae ni Raisi wa zamani wa nhi hiyo kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu.
Matokeo hayo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo yalionyesha kua mpinzani wa Bw Gbagbo, Alassane Outtara alikua ameshinda.

Laurent Gbagbo Raisi wa zamani wa Ivory Coast

Bi Simmone na mumewe walikamatwa mwaka 2011na kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC .
Hata hivyo Bw Gbagbo bado anasubiri hukumu yake katika mahakama hiyo


No comments: