VIINGILIO MECHI YA WATANI VYATANGAZWA

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limetangaza viingilio kwenye pambano la watani wajadi Yanga na Simba litakalopigwa kesho kwenye uanja wa Taifa jijini Dar es salaam majira ya saa kumi kamili za jioni kwa saa za Afrika mashariki.

Viingilio vya mchezo huo vitakuwa kama ifuatavyo, VIP A 40,000, VIP B 30,000, VIP C 20,000, viti vya rangi ya machungwa (Orange) 10,000 na viti vya rangi ya kijani na bluu ikiwa ni shilingi 7000



Mpambano hua utachezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro, akisaidiwa na Soud Lila wa Dar es salaam, mshika kibendera wa kwanza ni Florentina Zabroni kutoka Dodoma, mshika kibendera wa pili ni Israel Mjuni kutoka Dar es salaam na kamisaa wa mchezo ni Ame Santimeya kutoka Dar es salaam


Ikumbukwe mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikua ni disemba mwaka jana katika pambano la Nani mtani jembe ambapo Simba ilishinda kwa mabao mawili kwa sifuri 











No comments: