FAMILIA ZAENDA KUTAMBUA MIILI YA WANAFUNZI WALIOWAWA KENYA

Familia za wanafunzi waliouawa katika chuo kikuu kaskazini mashariki mwa Kenya zimeenda katika eneo la mkasa ili kuitambua miili ya waliouawa.








Zaidi ya watu 140 waliuawa katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Al shabaab mjini Garissa siku ya alhamisi ambapo wapiganaji hao waliwatenganisha wanafunzi hao kwa misingi ya kidini kabla ya kuwaua wanafunzi wa kikristo.


Wakati huohuo mamlaka nchini Kenya imetoa mabasi ili kuwasafirisha wanafunzi walionusurika hadi makwao,huku miili ya waliofariki ikisafirishwa hadi mjini Nairobi.


Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamoud,amesema kuwa Somalia na Kenya lazima ziimarishe ushirikiano wao dhidi ya Ugaidi baada ya shambulizi hilo.

Hili ni shambulio kubwa zaidi la pili kuwahi kufanywa na kundi la kigaidi la Al Shabab katika nchi ya Kenya ikumbukwe mwaka 2013 kundi hilo lilifanya shambulio katika eneo la Westget Mall jijini Nairobi


No comments: