CHARLES HILLARY NIKO TAYARI KUWAFUNDISHA VIJANA JINSI YA KUTANGAZA MPIRA

Mtangazaji mkongwe wa kituo cha BBC London Mtanzania Charles Hillary maarufu kama "Anko" amesema kuwa kitu ambacho atapendelea kukifanya wakati huu anapoachana na kazi ya kutangaza mpira ni kuwafundisha watangazaji vijana jinsi ya kutangaza mpira.


















Charles Hillary aliyasema hayo leo mara baada ya kumalizika kwa 
pambano la ligu kuu ya England kati ya Arsena na Liverpool ambalo lilikuwa ni pambano lake la mwisho kulitangaza akiwa mtangazaji maarufu wa mpira wa idhaa ya kiswahili ya BBC London.

"Watangazaji wengi wa sasa wa mpira hususani vijana wamekuwa wakipiga kelele  nyingi wakati wa utangazaji wao hivyo basi nitapendelea zaidi kuwapa mafunzo jinsi gani ya kutangaza mpira kwani kutangaza mpira hakuhitaji kupiga kelele saana" Alisema Hillary.


Charles Hillary ambae ametangaza rasmi  kuachana na kazi ya utangazaji mpira ambayo ameitumikia kwa zaidi ya miaka 30 ambapo pambano lake la kwanza kutangaza ilikuwa ni kwenye mchezo kati ya Yanga na Costal Union ya Tanga kwenye uwanja wa Taifa (sasa uhuru) mwaka 1982 kipindi hicho akiwa mtangazaji wa Redio Tanzania.








No comments: