Kiungo mahili wa fc Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Xavi Hernandez anatarajiwa kuagwa leo atakapokuwa anacheza mechi yake ya mwisho ya ligi kuu ya Hispania la liga wakati Barcelona itakapowakaribisha depotivo la coruna katika dimba la Nou camp kwenye mechi ya mzunguko wa mwisho wa ligi hiyo.
Kiungo huyo hodari amezaliwa January 25 mwaka 1980 katika kijiji cha Teresa kilichopo Barcelona kwenye jimbo la katalunya ni zao la lakituo cha kukuzia vipaja cha klabu hiyo kijulikanacho kama La Masia ambacho alijiunga nacho mwaka 1991 akiwa na umri wa miaka 11.
Xavi alianza kuichezea timu ya vijana ya Barcelona aliyoichezea jumla ya michezo 61 kuanzia mwaka 1991 hadi mwaka 1997, kuanzia mwaka 1998 alipandishwa kikosi cha kwanza cha Barcelona kilichokuwa kinanolewa na kocha wa sasa wa man utd Luis van gaal na mechi yake yakwanza ilikua dhidi ya real Mallorca agusti 18 1998 ambapo Barcelona ililala kwa mabao 2-1 huku bao hilo la barca akilifunga yeye.
Kiungo huyo ambae anatajwa kama kiungo bora wa kati hodari zaidi kwa kupiga pasi aliewahi kutokea katika ulimwengu wa soka amefanikiwa kuichezea Barcelona mechi zaida ya 700 na huku akifunga mabao 82 na kufanikiwa kutwaa jumla ya vikombe 25 akiwa na klabu.
Kwa upande wa timu ya taifa ya Hispania Xavi ameichezea timu hiyo kwenye levo mbalimbali kama vikosi vya vijana chini ya miaka 17,18, 20, 21, 23 na kikosi cha wakubwa ambapo amefanikiwa kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo kombe la dunia pamoja na kombe la ulaya maarufu kama euro.
No comments:
Post a Comment