Mtangazaji maarufu wa kipindi cha dira ya dunia kinachorushwa na idhaa ya kiswahili ya bbc London salim kikeke ameibuka mshindi katika kategori ya mtangazaji wa luninga anaependwa zaidi katika tuzo za watu kwa mwaka 2015.
Katika hafla ya ugawaji wa tuzo hizo iliyofanyika jana kikeke aliwashinda watangazaji mbalimbali aliokuwepo nao kwenye kategori hiyo ambao ni salama jabir, Dulla ambua na Sam misago wa east Africa TV pamoja na zamaradi mketema wa clouds tv.
Katika hatua nyingine mtangazaji wa clouds fm Millard ayo amechukua tuzo ya blogu/tovuti inayopendwa zaidi kupitia tovuti yake ya Millard ayo.com akizishinda blogu na tovuti nyingine kama michuzi blog zilizokuwepo kwenye kategori hiyo.
Kwa upande wa wasanii msanii wa kizazi kipya Ali kiba amechukua tuzo ya msanii wa kiume anaependwa zaidi huku kwa upande wa wanawake tuzo hiyo ikienda kwa msanii lady jaydee.
Hivi ni vipengele vyote pamoja na washindi wa tuzo hizo
Mtangazaji wa redio anaependwa
D' jaro arungu TBC FM
Kipindi cha redio kinachopendwa
Papaso TBC FM
Mtangazaji wa runinga anaependwa
Salim kikeke BBC SWAHILI
Kipindi cha runinga kinachopendwa
Mkasi EATV
Blogu/ tovuti inayopendwa
Millard ago.com
Muongozaji video anaependwa
Hasscana.
Muongozaji filamu anaependwa
Rey kigosi
Muigizaji filamu wa kike anaependwa wema sepetu
Muigizaji filamu wa kiume anaependwa
Hemedy PhD
Msanii wa muziki wa kiume anaependwa
Ally kiba
Msanii wa muziki wa kike anaependwa
Lady jaydee
Filamu inayopendwa
Kigodoro
Video ya muziki inayopendwa
Nani kama mama
Christian bella ft Omy dimpozi.
No comments:
Post a Comment