Swansea imekua timu ya tatu katika historia ya ligi kuu ya England kuzifunga Man U na Arsenal nyumbani na ugenini ndani ya msimu mmoja
Timu nyingine ni West Ham 2006/07 na Chelsea 2009/10
Hull city ambayo imeshuka daraja haikuwahi kushinda mechi yoyote kipindi cha mwezi Mei kwenye ligi kuu ya England imedroo 4 na kufungwa 9.
Makocha wa timu nne ambazo zimeifunga Chelsea msimu huu majina yao yameanziwa na herufi P makocha hao ni Pardew(Newcastle), Pochettino(spurs), Pullis (west brom) na Parkinson(millwool).
Chelsea imekuwa timu yakwanza katika historia ya ligi kuu ya England kupoteza mechi chache kwenye msimu mmoja mechi nne tu.
Sadio mane wa southampot ameweka rekodi ya kufunga magoli matatu (hat-trick) ya haraka zaidi kwenye historia ya ligi kuu ya England kwenye mechi dhidi ya Aston Villa dk 2 na sekunde 59.
Olivier Giroud wa Arsenal amefunga magoli katika mechi sita mfululizo za ligi kuu ya england kipindi cha mwezi Feb hadi Apr ni mchezaji wa kwanza kufanya hivyo tangu msimu wa 2008/09 alipofanya Emmanuel Adebayor.
John Terry wa Chelsea ameweka rekodi ya beki aliefunga magoli mengi zaidi kwenye historia ya ligi kuu England magoli 39.
Southampton imekuwa timu yakwanza katika historia ya ligi kuu England kufunga magoli matano ndani ya kipindi cha kwanza na magoli matoni ndani ya kipindi cha pili kwenye mechi mbili tofauti ndani ya msimu mmoja mechi dhidi ya Sundarland na mechi dhidi ya Aston Villa.
Diego Costa amekuwa mchezaji wa nne wa Chelsea kufunga mabao 20 ndani ya msimu mmoja wa ligi kuu England wengine ni Lampard, Drogba na Hasellbank.
Alex Sanchez amefikia rekodi iliyowekwa na Thiery Henrry ya kufunga mabao 20 kwenye msimu wa kwanza kuichezea klabu hiyo.
Wayne Rooney wa Man Utd ameweka rekodi yakuwa mchezi wa kwanza kufunga mabao 10 kwenye misimu 11 mfululizo ya ligi kuu ya England.
No comments:
Post a Comment