IDADI YA VIFO VILIVYOTOKANA NA MVUA YAFIKIA 12

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kupitia kwa kamishina wa jeshi hilo Suleimani Kova limetoa taarifa ya kuongezeka kwa vifo vilivyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam kuwa imefikia vifo kumi na mbili(12).

Katika taarifa hiyo iliyotolewa jana na jeshi hilo imeorodhesha majina ya marehemu waliookotwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ambao ni VALERIAN  ERADIUS, Miaka 13, Mwanafunzi wa kidato cha
kwanza, shule ya sekondari Kigogo, Mkazi wa Mburahati kwa Shebe, GERVAS  SHAYO, Miaka
28, shamba boy, mkazi wa Mbezi juu wilaya ya kinondoni.

Maiti nyingine mbili hazikuweza kufahamika majina ambazo moja niyamwanamke anaekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40-45 iliyookotwa katika bonde la mto Mkwajuni,
mtaa wa Makuti, Magomeni wilaya ya kinondoni na nyingine ya mwanaume anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35-38 iliyookotwa  maeneo ya Magomeni Suna katika bonde
la Mto Msimbazi.

Taarifa hii ya jeshi la polisi imeonyesha ongezeko la vifo vya watu wanne (4) baada  ya taarifa ya awali ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari kunyesha idadi ya watu waliopoteza maisha kuwa ni watu nane(8).

Hata hivyo jeshi hilo limewataka wananchi kuzingatia taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini ili kupunguza athari zinazotokana na mvua.

No comments: