Timu ya fc Barcelona Jana usiku ilifanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa ulaya licha yakufungwa na Bayern munichen ya ujerumani kwa jumla ya mabao matatu kwa mawili
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la alianz arena ambao ni uawnja wa fc Bayern, wenyeji hao ndio walikuwa wakwanza kupata bao kwenye dakika ya 7 kipindi cha kwanza lililofungwa na beki mehid benatia akiunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na xabi alonso.
Bao hilo lilidumu kwa dakika nane tu kwani katika dakika ya 15 neymar aliisawazishia Barcelona baada yakupokea pasi safi kutoka kwa Luis Suarez, neymar aliipatia Barcelona bao la pili akiunganisha vizuri pasi ya Luis Suarez katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili Bayern walifanikiwa kupata mabao mawili yaliyofungwa na Robert Lewandowsk kwenye dakika ya 59 na Thomas Muller dakika ya 74 ambayo yaliwapa ushindi fc Bayern.
Matokeo hayo yameifanya fc Barcelona ifuzu kwenda hatua ya fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3 kwani katika mechi ya kwanza iliopigwa kwenye dimba la Camp now Barcelona walipata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.
Nusu fainali nyingine inatarajiwa kupigwa leo pale Real Madrid ya Hispania itakapowakaribisha kibibi kizee cha Turin timu ya Juventus ya Italia kwenye uwanja wa Santiago bewenye mechi ya kwanza iliopigwa nchini Italia juve ilpata ushindi wa mabao 2-1 hivyo watahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili waweze kufuzu hatua ya fainali.
No comments:
Post a Comment