Kocha mkuu wa timu ya Real Madrid ya Hispania muitaliano Carlo Ancelort amesema kuwa hana uhakika kama ataendelea kuifundisha miamba hiyo ya Hispania kutokana na matokeo ya klabu hiyo msimu huu.
Kauli hiyo ameitoa baada ya klabu hiyo kushindwa kufuzu fainali ya klabu bingwa ulaya hapo jana kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na juventus ya Italia kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya.
"Zimebaki siku 15 na tumebakisha mechi 2 tu msimu kuisha badala ya hapo nitaongea na uongozi kujua hatima yangu" Alisema Ancelort ambae msimu uliopita aliiwezasha real Madrid kutwaa taji la 10 la klabu bingwa ulaya.
Real Madrid ipo nyuma kwa tofauti ya pointi 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Hispania La liga huku vinara wakiwa ni mahasimu wao klabu ya fc Barcelona ambayo imetinga fainali ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kuitoa Bayern munichen ya ujerumani.
No comments:
Post a Comment