Wakimbizi wawili wameripotiwa kufariki dunia mkoani kigoma ilipo kambi ya wakimbizi wanaotoka nchini Burundi kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Leonald Subi alisema mjini Kigoma kwamba watu wawili walikufa wakiwa tayari wanaumwa ugonjwa huo na alisema watu wawili wengine, walipatwa na ugonjwa huo wakisubiri msaada wa kibinadamu katika kijiji cha Kagunga wilaya Kigoma, mwambao wa Kaskazini wa Ziwa Tanganyika.
Subi alisema kuwa kwa sasa hali ya upatikaji wa huduma za kibinadamu, ikiwemo chakula, maji, mahala pa kujihifadhi na huduma ya choo ni mbaya sana kutoka na idadi kubwa ya wakimbizi hao kuwepo kijijini hapo kwa kipindi kifupi na hivyo kijiji hicho kuzidiwa katika kuwapatia huduma watu hao.
No comments:
Post a Comment