Mwigizaji maarufu wa filamu kutoka nchini Kenya Lupita Nyong'o amepata nafasi ya kuigiza kwenye muvi za Hollywood series baada ya kufanikiwa kuwemo kwenye sinema inayoitwa STAR WARS EPSOD VII "The force awakens".
Mwigizaji huyo kutoka nchini Kenya alitambulika kwenye ulimwengu wa filamu baada ya kuigiza vizuri kwenye sinema yake ya kwanza na iliyompa umaarufu iitwayo " 12 Years as a slave" ambayo pia ilimfanya apate tuzo ya mugizaji bora wa kike kutoka Afrika kwenye tuzo za OSCAR mwaka jana.
Kwenye filamu hiyo ya STAR WARS iliyoigizwa nchini Marekani Lupita ameigiza kama Asajj Ventress akishirikiana na nyota wakubwa wa filamu duniani kama vile mmarekani Harrison Ford na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment