MVUA YAUWA NANE DAR

Watu nane wameripotiwa kufa pamoja na mamia kukosa makazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji jijini Dar es salaam kufuatia mvua kali zinazoendelea kunyesha nchini.

Mvua hizo ambazo zinaendela kunyesha zimesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu pamoja na baadhi ya wananchi hususani wa mabondeni kukosa mahali pakuishi kutokana na nyumba zao kwenda na maji.

Pia mvua hizo zimesababisha kuwepo kwa msongamano mkubwa wa magari hali ambayo inasababisha wananchi kuchelewa kwenda pamoja na kurudi kwenye mishuhuliko yao yakila siku.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imetahadharisha kuwa mvua hizo zitaendelea kunyesha japo zitapungua kidogo.

No comments: