Pazia la ligi kuu ya vodacom Tanzania bara linatarajiwa kufungwa rasmi leo hii kwa timu zote 14 zinazoshiriki ligi hiyo kushuka dimbani kwenye mechi za mzunguko wa mwisho zitakazopigwa kwenye viwanja tofauti nchini.
Ligi hiyo ambayo bingwa pamoja na nafasi ya pili wakiwa wameshajulikana kivumbi kitakua kwenye time nne ambazo zinajikwamua na janga la kushuka daraja.
Timu hizo ambazo ni stendi united yenye pointi 28, mgambo jkt pointi 28, ndanda fc pointi 28, na Tanzania prison yenye pointi 28.ambapo timu mbili kati yao zitaungana na polisi morogoro ambao wenyewe wameshashuka daraja kuipa mkono wa kwa heri ligu kuu.
Ratiba ya mechi hizo ipo kama ifuatavyo
Kagera Sugar vs
Tanzania Prisons
JKT Ruvu vs Simba SC
Mbeya City vs Polisi Morogoro
Azam vs Mgambo JKT
Stand United vs Ruvu Shooting
Ndanda vs Young Africans
Mtibwa Sugar vs
Coastal Union
Mechi hizi zote zinachezwa siku moja na mda mmoja ili kuhofia upangaji wa matokeo
No comments:
Post a Comment