JERRY MURO "JAMANI TUWE WAZALENDO KWENYE MECHI ZA KIMATAIFA"

Timu zikenda kwenye michuano ya kimataifa basi tupeane support na michuano hiyo ikiisha turudi kwenye upinzani wetu kama kawaida.Tusipeleke upinzani wetu kwenye mashindano ya kimataifa tutakosa vitu muhimu ambavyo vinaleta tija kwa taifa.

Sisi Yanga tutabadilika na tunaomba vilabu vingine vibadilike, maana hata wenzetu kule Tunisia walitucheka kwamba wao walipata mashabiki wengi walivyokuja huku lakini sisi kule hatukupata hata mmoja. Hivyo sisi tutaanza kwa kudilika na wengine wafuatie.

Kuhusu usajili zinaandikwa habari nyingi kuhusu usajili wa Yanga. Sisi kama Yanga bado hatujapokea taarifa yoyote kutoka kwa mwalimu kama anamuhitaji mchezaji yoyote. Sasa hivi waandishi tunaomba mtusaidie ku- stablelize mshikamano wetu kama Yanga.

Sisi kama timu tumejiandaa kama timu ya kawaida, kuna habari kwamba ilitolewa kwamba Yanga imepanga matokeo kwa mechi mbili zilizobaki. Sio kweli kabisa sisi kama Yanga tutacheza kama kawaida, kuchukua ubingwa kabla ya mechi mbili sio sababu ya sisi kwamba tutapanga matokeo. Mechi itachezwa kama kawaida

No comments: