Mahakama yamruhusu Nkurunziza kugombea uraisi

Mahakama ya katiba nchini Burundi imemruhusu raisi was nchi hiyo anaemaliza muda wake Pierre Nkurunziza kugombea nafasi hiyo kwa muhula wa tatu

Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .

Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse ,alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.
Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali

No comments: