Msanii na muandaaji nyota wa muziki David Guetta amepata shavu kutoka shirikisho la soka barani ulaya Uefa kwa kupewa nafasi ya kuandaa wimbo maalumu kwaajili ya fainali za mataifa ya ulaya (Uefa Euro) zinazotarajiwa kutimua vumbi kuanzia mwezi Juni mwakani nchini Ufaransa.
Msanii huyo kutoka nchini ufaransa amepewa nafasi ya kuuandika na kuutengeneza wimbo huo maalumu ambao utaanza kutumika kwenye maandilizi ya michuano hiyo mapema mwakani na pia amepewa nafasi ya kutumbuiza kwenye mchezo wa ufunguzi kwenye uwanja wa Stade de France tarehe 10 Juni mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupewa nafasi hiyo Guetta alisema" nimefurahi sana kuwa sehemu ya michuano hii mikubwa kabisa kwa ngazi ya vilabu barani ulaya ambayo inafanyika katika ardhi ya nyumbani kwani mpira na muziki vinakwenda pamoja katika swala la burudani hivyo naahidi nitaifanya michuano hii kua kati ya michuano ambayo haitasahaulika" Alimaliza Guetta.
Nae kwa upande wake Raisi wa shirikisho la soka barani ulaya Uefa Michael Plattin amesema kuwa wameamua kufanya kazi na David Guetta kwa kuwa wanaamini kipaji chake na ni msanii ambae amejijengea umaarufu katika kazi yake ya muziki.
No comments:
Post a Comment