Gwiji wa soka kutoka brazili Arthur Antunes Coimbra maarufu kama Zico ametangaza rasmi kugombea nafasi ya uraisi kwenye shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huu mara baada ya raisi wa shirikisho hilo kujiuzulu kutokana na kashifa za rushwa zinazoikba shirikisho hilo.
Akizungumza na kundi kubwa la waandishi wa habari katika kituo chake cha kufundisha soka huko mjini Rio de Janerio, Zico amesema ni huzuni kwenye michezo kuona kile kinachotokea katika soka leo hii.Kuona rushwa, lakini pia kuona uchapakazi unaofanywa na baadhi ya watu wazuri ukipotezwa.Pia aliongeza kuwa, ni wajibu wake sasa kutumia uzoefu na ujuzi wake kujaribu kugombea urais wa shirikisho hilo kubwa duniani.
Hivi karibuni rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter, alitangaza kuwa atajiuzuru wadhfa wake huo ikiwa ni siku nne tu baada ya kuchaguliwa tena kushika madaraka hayo. Uamuzi huo wa Blatter ulikuja ikiwa ni siku chache tu baada mamlaka ya Marekani na Uswiz kufungua kesi ya rushwa ya kwa baadhi ya maafisa wa FIFA.
Zico, 62, aliyecheza katika fainali tatu za Kombe la Dunia, alihudumu kama waziri wa michezo Brazil miaka ya 1990 na ana uzoefu katika ngazi zote za mchezo huo ikiwa ni pamoja na vipindi vya ukufunzi Japan, Uturuki, Urusi, Ugiriki na Mashariki ya Kati.
No comments:
Post a Comment