Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho Gaucho amesema kuwa mchezaji mpya aliesajiliwa hivi karibuni na klabu ya Liverpool mbrazil Roberto Firmino atatengeneza combination ya kutisha na mbrazil mwenzake aliyopo klabuni hapo Phillipe Coutinho
Gaucho aliyasema hayo juzi baada ya majogoo wa jiji Liverpool kukamilishi uhamisho wa Firmino aliekua anakipiga katika klabu ya Hoffenheim inayoshiriki ligi kuu ya ujerumani maarufu kama bundersliga kwa kitita cha Euro milioni 29.
Gaucho alisema kua Liverpool kumpata Firmino kwao nikitu kizuri sana kwani kwa kushirikiana na Coutinho watatengeneza moja kati ya safu bora ya kiungo barani ulaya kwani wote wana vipaji na wana uwezo wa kucheza namba zote za mbele.
Gaucho pia aliongeza na kusema kua ukitazama vipaji, ubunifu na uwezo waliokuwa nao vijana hawa ni dhahiri kuwa wataisadia na kuibadilisha sana Liverpool na nimoja kati ya usajili mzuri wa Liverpool kwa msimu huu.
Robert Firmino ameichezea Hoffenheim jumla ya michezo 152 na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 49 tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea nchini kwao Brazil mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment