KIIZA AWA BEST MAN WA OKWI

Mshambuliaji wa zamani wa yanga raia wa Uganda Hamsi Kiiza juzi alikua msimamizi (best man) wakati mganda mwenzie ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya simba Emmanuel Okwi alipokuwa anafunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi Frolence Nakalegga.

Sherehe hiyo iliyofanyika juzi Julai 27 mwaka huu jijini Kampala nchini Uganda ilihudhuriwa na watu wengi mashuhuri akiwemo kocha wa timu ya taifa ya Uganda Mserbia
SREDOJEVIC MILUTIN 'MICHO' pamoja na maofisa wakuu wa jeshi. 

Awali Okwi aliwahi kufunga ndoa ya kimila kwa ajili ya kumtambulisha mpenzi wake huyo kwa wazazi wake.

No comments: