Mchezaji bora wa msimu huu kwenye ligi ya kikapu nchini Marekani NBA Stephen carry alfajiri ya leo aliiongoza timu yake ya Golden state woriours kutwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kusubiri kwa kipindi cha miaka 40.
Kwenye mchezo huo ambao ulikua ni wa mzunguko wa 6 kati ya mizunguko 7 ya michezo ya fainali ya ligi hiyo Wariours waliifunga Clevarland cavaries kwa jumla ya vikapu 105-96 na Carry kufunga jumla ya vikapu 25
Huo ni ushindi wa 4 mfululizo kwa Wariours baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo kwenye mzunguko wa kwanza na wapili hivyo kwa jumla Wariours wanakuwa wameshinda mizunguko 4 kati ya 6 ambayo wamecheza mpaka sasa na wapinzani wao Cavs wameshinda mizunguko 2.
Mchezaji nyota wa timu ya Clevarland Lebron James alifunga jumla ya vikapu 36 kwenye mchezo huo lakini havikuweza kuisaidia timu yake. Kwa sasa umebaki mchezo mmoja wa mzunguko wa 7 ambao utakua ni wakukamilisha ratiba kwani hata Cavs wakishinda hawawezi kufikia mizunguko ya Woriours.
No comments:
Post a Comment