MAKUBALIANO YA KUKOKOA UCHUMI WA UGIRIKI YAFIKIWA

Ugiriki na wakopeshaji wake wamefikia makubaliano juu ya mpango mpya wa uokoaji wa uchumi wake , vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti leo, kufuatia wiki mbili za majadiliano makali.

Pande hizo mbili zimekuwa katika mvutano kukamilisha makubaliano hayo na kuipa Ugiriki nafasi ya kupata fedha za kuuokoa uchumi wake ifikapo Agosti 20, wakati ikitarajiwa kulipa deni la kiasi cha euro bilioni 3.2 kwa benki kuu la Ulaya.

Waziri wa fedha wa Ugiriki Euclides Tsakalotos amewaambia wandishi habari mjini Athens ,kwamba bado kuna mambo mawili matatu ya kufafanua.
Lakini vyombo vya habari vya Ugiriki vimenukuu duru za serikali zikisema kwamba makubaliano yamefikiwa katika tamko la makubaliano , ambalo litaeleza hatua za kiuchumi zilizoahidiwa kutekelezwa na Ugiriki ili kupata msaada huo wa uokozi.

Afisa wa Ujerumani akizungumza na kituo cha taifa cha televisheni ARD , amesema nafasi inaonekana kuwa nzuri kupatikana makubaliano ya mwisho kuhusu makubaliano hayo.

No comments: