Bunge la Iraq limepiga kura kwa wingi ili kuunga mkono mapendekezo yaliotolewa na Waziri Mkuu Haider al Abadi ,kwa lengo la kukabiliana na ufisadi pamoja na kupunguza matumizi ya serikali.
Spika wa bunge hilo Salim al Juburi alisema kuwa mswada huo umepitishwa bila upinzani wowote.
Mpango huo unashirikisha kupunguzwa kwa baadhi ya nyadhfa serikalini, kumaliza ubaguzi wa kidini pamoja na ule wa kisiasa wakati wa kutolewa kwa ajira serikalini mbali na kuanzisha uchunguzi dhidi ya ufisadi.
Chazo – BBC
No comments:
Post a Comment