MAN CITY WAANZA KWA KISHINDO ENGLAND

Mabingwa wa zamani wa England, Manchester City wameanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu kwa ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya West Bromwich Albion usiku wa kuamkia leo.

Shujaa wa mechi alikuwa ni kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure aliyefunga mabao mawili, lingine likifungwa na nahodha wa timu hiyo Vincent Kompany.

Mwanasoka bora Afrika, Yaya Toure alianza kuifungia Manchester City dakika ya tisa baada ya shuti lake la umbali wa mita 20 kumbambatiza golokipa wa West brom  Boaz Myhill na kutinga wavuni, kabla ya kufunga la pili dakika ya 24.
Nahodha wa Man City, Vincent Kompany akakamilisha ushindi mnono katika mchezo wa kwanza wa timu yake kwa kufunga bao la tatu dakika ya 59 kwa kichwa.

Mchzeaji mpya, Raheem Sterling aliyesajiliwa kutoka Liverpool, alicheza vizuri katika kikosi cha City jana, lakini akapoteza nafasi nzuri na ya wazi ya kufunga.
Kikosi cha West Brom kilikuwa: Myhill, Chester, Dawson, Lescott, Brunt, Morrison, Gardner, Fletcher, McClean/Yacob dk46, Lambert/Anichebe dk73 na Berahino/ dk79.

Man City; Hart, Sagna, Kompany, Mangala, Kolarov, Toure/Demichelis dk79, Fernandinho, Jesus Navas, Silva, Sterling/Nasri dk73 na Bo.Dk 62.

No comments: