TAKWIMU NA REKODI ZILIZOWEKWA KWENYE MECHI ZA UFUNGUZI WA LIGI KUU YA ENGLAND MSIMU WA 2015/2016.

Msimu mpya wa ligi kuu ya England umeanza wikiendi iliyopita na kumalizika siku ya  jumatatu kwa mechi za ufunguzi wa ligi hiyo baada ya timu zote 20 zinazoshiriki ligi hiyo kushuka dimbani siku ya jumamosi, jumapili na jumatatu.
Hizi ni baadhi ya takwimu na rekodi zilizowekwe na wachezaji pamoja na timu kwenye mechi za ufunguzi wa ligi hiyo.

MAN U 1-0 SPURS

Hii ni Mara ya kwanza katika historia ya ligi kuu ya England goli la ufunguzi kua nilakujifunga hii ni mara baada ya mlinzi wa Tottenham Hotspur Cairl Warker kujifunga goli ambalo liliwapatia Man utd ushindi.

Man utd wamefanikiwa kupata ushindi bila wavu wao kuguswa katika mechi ya ufunguzi, hii ni Mara ya kwanza tangu 2010 walipoifunga Newcastle 3-0.

Man utd wamepoteza mechi moja tu kati ya 24 za ufunguzi walizocheza kwenye dimba la old Trafford wameshinda 17 na kutoa sare 6.

Kwa Mara ya pili katika historia ya spurs kujifunga goli kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu England baada ya Ramon Vega kufanya hivyo mwaka 1997.

BOURNAMOUTH 0-1 A.VILA

Aston Villa wamepata ushindi kwenye mechi ya ufunguzi kwa mara ya kwanza dhidi ya timu iliyopanda daraja kwenye historia ya EPL.

Katika mechi 7 zilizopita za Aston Villa walizocheza ugenini hawakuruhusu wavu wao kuguswa.

Mshambuliaji wa Aston Villa Ruddy Gestede amefunga magoli katika mechi 5 mfululizo za EPL kwenye historia yake.

EVERTON 2-2 WATFORD

Kiungo wa evarton Ross Bakley amefunga magoli katika mechi zote za ufunguzi alizocheza kwenye ligi kuu England na magoli yote ameyafunga akiwa kwenye eneo la nje ya kumi na nane.

Everton wamepata sare ya 2-2 kwenye mechi tatu mfululizo za ufunguzi wa ligi kuu England.

Kwenye mechi zote tano walizokutana Everton na Watford kulipatikana goli katika dakika 5 za mwisho.

LEICESTER 4-2 SUNDALAND

Klabu ya Leicester imeshinda mechi 5 na kupoteza moja kwenye mechi 6 za karibuni kwenye ligi kuu England.

Mshambuliaji wa Sunderland Jamien Defoe amefunga magoli kwenye misimu 15 ya ligi kuu England na sasa amefikisha idadi ya mabao 129.

Tangu  kuanza kwa mwezi Aprili mwaka huu klabu ya Leicester imekusanya pointi nyingi kuliko klabu yoyote ya ligi kuu England pointi 25.

NORWICH 1-3 CRYSTAL PALACE

Mshambuliaji wa Palace Wilfred Zaha amefunga magoli 3 kwenye mechi 5 zilizopita za ligi kuu England.

Kocha wa Palace Alan Pardew ameshinda idadi kubwa ya mechi akiwa na klabu hiyo katika historia ya ligi kuu England ameiongoza kwenye mechi 19 na ameshinda mechi 11.

Kiungo wa palace Yohan Kabaye amefunga goli lake la 18 katika ligi kuu England huku magoli 6 kati ya hayo akiwa ameyafunga kwenye mechi 8 za karibuni.

CHELSEA 2-2 SWANSEA

Swansea imekua timu ya kwanza kufunga magoli mawili katika dimba la Stanford Bridge katika historia ya ligi kuu England baada ya kufanya hivyo mwezi septemba mwaka wa jana walipofungwa magoli 4-2.

Bafetimbi Gomis amekua mchezaji wa pili baada ya Steven Naismith wa Everton kuzifunga timu za Chelsea, man utd, man city na arsenal katika misimu miwili ya ligi kuu England.

Magoli 3 aliyofunga Oscar kwenye mechi 8 zilizopita za ligi kuu England ameyafunga dhidi ya Swansea.

Chelsea haijapoteza mchezo hata mmoja kati ya 17 ya ufunguzi iliyocheza tangu msimu wa 1998/99. Wameshinda 14 na kutoka sare 3.

ARSENAL 0-2 WEST HAM

West ham wamevunja uteja wa kufungwa katika mechi 9 mfululizo za ligi kuu England na klabu ya Arsenal.

Reece Oxford wa west ham ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenyewe umri mdogo kucheza mechi ya ligi kuu England miaka 16.

Arsenal hawajafunga goli hata moja kwenye mechi 4 kati ya 5 zilizopita za ligi kuu England kwenye uwanja wao wa nyumbani Emirates.

Ushindi wa west ham dhidi ya arsenal juzi ulikua ushindi wa kwanza tangu mwaka 2007 walipoipa arsenal kichapo cha kwanza kwenye uwanja wao mpya wa Emirates.

NEWCASTLE 2-2 SOUTHAMPTOpark Newcastle wamefunga magoli 15 kwenye mechi 16 dhidi ya Southampton kwenye uwanja wao wa nyumbani st James park kwenye ligi kuu England.

Southampton wameruhusu magoli mawili kwenye kila mechi, Katika mechi 5 zilizopita za ligi kuu England.

Mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle amefunga magoli mawili tu kwenye mechi za ugenini alizoichezea Southampton.

STOKE 0-1 LIVERPOOL

Huu ni ushindi wa Liverpool katika mechi 5 za ugenini kwenye ligi kuu England tangu mwezi machi  wametoka sare 2 na kupoteza 3.

Magoli yote 5 aliyofunga Fillipe Coutinho ndani ya mwaka 2015 kwenye ligi kuu England ameyafunga akiwa nje ya kumi na nane.

WEST BROWM 0-3 MAN CITY

Man city wameshinda mechi 7 mfululizo za ligi kuu England, mwenendo mzuri zaidi tangu mwaka 2014. 

Yaya Toure amefunga magoli 5 kwenye mechi 3 za mwisho kwenye uwanja wa nyumbani wa west brom the horthons.

Man city wamepiga jumla ya pasi sahihi 696 kwenye mechi hii 221 zaidi ya timu zote zinazoshiriki ligi kuu England kwenye mechi za ufunguzi.

Takwimu na rekodi hizi zinatokana na mechi za ufunguzi wa ligi kuu England je zitaendelea kudumu hadi mwisho wa msimu? Mm na wewe hatujui cha msingi ni kurndelea kufuatilia ligi kuu ya England na kutembelea blog hii ili uweze kupata updates zote za kimichezo.


No comments: