MESS, INIESTA WAIFIKIA REKODI YA XAVI BARCELONA

Wachezaji Leonel Mess na Andress Iniesta wa fc Barcelona ya Hispania jana usiku waliiwezesha klabu yao kutwaa ubingwa wa  uefa cup baada ya kuwafunga ndugu zao wa Hispania klabu ya sevilla kwa mabao 5-4.

Kwa ubingwa huo Mess na Iniesta wamefikia rekodi ya Kiungo mkongwe aliyeichezea klabu hiyo kwa mafanikio makubwa Xavi Hernandez kutwaa jumla ya mataji 25 ndani ya klabu hiyo.

Mechi hiyo iliyopigwa jana usiku kwenye dimba la tbllis nchini Georgia Barca walishinda kwa mabao 5-4 katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 mechi hiyo kumalizika kwa mabao 4-4.

Kwenye mchezo huo ambao huwakutanisha mabingwa wa klabu bingwa barani ulaya na mabingwa wa kombe la ueropa, sevilla ndio walikua wa kwanza kupata bao katika dk ya 3 lililofungwa na Ever Banega lakini bao hilo lilidumu kwa dakika 4 tu kwani katika dk ya 7 Leonel Mess aliisawazishia Barca kabla hajaongeza la pili katika dakika ya 16.
Kwenye dk ya 44 Barca walipata bao la 3 kupitia kwa Rafinha na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko barca wakiwa mbele kwa mabao 3-1.
Luis Suarez alifanikiwa kuifungia barca bao la 4 mnamo dk ya 56 kipindi cha pili kabla ya Reyes, Guamero na Kanoplyanka kuisawazishia sevilla na kufanya mchezo huo kwenda katika dakika 120 baada ya dk 90 kumalizika kwa 4-4.
Mshambuliaji wa Barcelona anaewindwa na klabu ya Manchester united Pedro Rodriguez aliifungia barca bao la 5 na laushindi katika mchezo kwenye dk ya 156.

Barcelona pia wamefikia rekodi ya klabu ya Ac Milan ya Italia kwa kutwaa kombe hilo kwa mara ya tano.

No comments: