MTOTO LOUIS DIAMOND APATA NAFASI YA KUONANA NA SHUJAA WAKE

Si unaikumbuka ile video iliyosambaa kwenye mitandao mingi duniani majuma kadhaa yaliyopita ikumuonyesha mtoto  mwenye  umri wa miaka mitano akilia kwa uchungu baada ya kupata taarifa kuwa mshambuliaji wa Man utd Robin Van Perse  ameuzwa kunako klabu ya Fernebache ya uturuki.

Mtoto yule ambae jina lake ni Louis Diamond amepata ofa ya kulipiwa usafiri yeye na familia yake na klabu ya Fernebache kwenda nchini Uturuki kumshuhudia shujaa wake Van Persea akikipiga katika klabu hiyo kwenye mechi ya ligi kuu ya Uturuki dhidi ya Eskisehirspor na Fernebache kushinda mabao 2-0.

Louis Diamond ni shabiki mkubwa wa Man United, lakini leo akiwa na wadogo zake amevaa jezi ya Fernabahce na kukutana na shujaa wake.
Ilikuwa furaha ya aina yake wakati alipojumuika live na van Persie ambaye alilimlilia kwa uchungu ile mbaya.

Diamond pia amepata nafasi ya kupiga picha na Van perse akiwa amevaa jezi ya Fernebache. Kwa sasa mtoto huyo anafuraha kubwa na wanajiandaa yeye na familia yake  kwaajili ya safari ya kurudi England.

No comments: