SERIKALI YAJA NA MPANGO HUU KUZUIA WIZI WA MADINI

Serikali inapoteza mapato mengi kutokana na utoroshwaji wa madini mbalimbali yanayopatikana hapa nchini hususani yale ya aina ya Tanzanite.
Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kuungana na nchi nyingine 12   kuandaa maabara maalumu zitakazoweza kutumia teknolojia ya alama ya vidole kugundua madili ya nchi husika hata kama yakitoroshwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika kongamano lililohusisha nchi za maziwa makuu duniani, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava amesema hatua hiyo itasaidia nchi husika kuanza kunufaika na mapato baada ya mauzo.

Hadi sasa maabara tatu zimeanza kujengwa katika nchi za Tanzania, Congo na Rwanda na kwa hapa nchini maabara hiyo itaanza kazi mwakani.

No comments: